toleo la kirafiki la simu bonyeza hapa MAFUNDISHO YA KUKATALIWA Doctrines to be Rejected 1. Kuwa Biblia ni kazi ya pumzi ya Mungu kwa sehemu tu—au ikiwa kamili, ina makosa ambayo pumzi hiyo imeyakubalia. 2. Kuwa Mungu ni utatu. 3. Kuwa Mwanga wa Mungu amekuwapo tangu mwanzo pamoja na Baba. 4. Kuwa Kristo alizaliwa akiwa na "maisha yasiyo na kizuwizi". 5. Kuwa maumbile ya Kristo yalikuwa safi. 6. Kuwa Roho Mtakatifu ni utu ulio tofauti mbali na Baba. 7. Kuwa mtu ana nafsi isiyokufa. 8. Kuwa mtu ana uhai katika hali ya mauti. 9. Kuwa waovu watateseka katika moto wa milele. 10. Kuwa wenye haki watapaa kwenda katika ufalme mawinguni wanapokufa. 11. Kuwa ibilisi ni janga lenye uwezo usio wa ulimwengu huu. 12. Kuwa Ufalme wa Mungu ni "kanisa". 13. Kuwa Injili sio zaidi ya kifo, kuzikwa, na kufufuka kwa Kristo. 14. Kuwa Kristo hatarudi tena hadi miaka elfu moja iishe. 15. Kuwa baraza ya hukumu ya Kristo atakapokuja, sio kuwahukumu watakatifu, bali ni kuwagawia viwango mbali vya ijara kati yao. 16. Kuwa ufufuo ni kwa waaminifu peke yao. 17. Kuwa waliokufa watafufuliwa wakwa na miili isiyoweza kufa. 18. Kuwa raia wa mataifa yatakayokuwapo katika miaka elfu moja watakuwa na miili isiyoweza kufa. 19. Kuwa sheria ya Musa ni lazima kwa wanaoamini Injili. 20. Kuwa kuishika siku ya Jumapili ni wajibu. 21. Kuwa kunyunyizwa kwa watoto wachanga ni mafundisho ya Maandiko. 22. Kuwa "mataifa yasiyoabudu Mungu", watu wazimu, wapaganis, na watoto wadogo wataokolewa. 23. Kuwa mtu aweza kuokolewa kwa uadilifu na uaminifu, pasipo Injili. 24. Kuwa Injili pekee itaokoa bila utii wa amri za Kristo. 25. Kuwa mtu hawezi kuamini asipokuwa na Roho wa Mungu. 26. Kuwa maisha ya wokovu kwa watu yameazimiwa kimbele bila hiari yao. 27. Kuwa hakuna dhambi katika mwili. 28. Kuwa Yusufu alikuwa baba haswa wa Yesu. 29. Kuwa dunia itaangamizwa. 30. Kuwa ubatizo si lazima kwa wokovu. 31. Kuwa maarifa ya ukweli sio lazima kuufanya ubatizo kuwa halali. 32. Kuwa nyama (au vyakula) fulani vikataliwe kwa sababu ya unajisi. 33. Kuwa Waingereza ndio makabila kumi ya Israeli, ambao kustawi kwao ni ishara ya kutimizwa kwa miadi iliyonenwa kuhusu Efrahimu. 34. Kuwa kufunga ndoa na asiyeamini ni halali. 35. Kuwa tu huru kutumika katika jeshi, au kama polisi, kushuriki siasa, au kutumia sheria kulazimisha kurudishiwa mali iliyoazimwa. AMRI ZA KRISTO The Commandments of Christ 1. Wapende adui zako; watendee mema wakuchukiao. (Mt. 5:44). 2. Usiwapinge waovu: mtu akikupiga shavu la kushoto, mpe na la kulia (Mt. 5:39, 40). 3. Usilipize kisasi: epukana na hasira: kubali kupata hasara (Rum. 12:18-19; 1 Kor. 6:7). 4. Mtu akichukua mali yako, usiulize urudishiwe (Luka 6:29-30). 5. Patana na adui wako upesi, hata kukubali makosa kwa ajili ya amani (Mt. 5:25; 1 Kor. 6:7). 6. Usisumbukie utajiri: kuwa tayari kutenda mema, wape wakuulizao: wasaidie wahitaji (1 Tim. 6:8; Rum. 12:13; Ebr. 13:16; Yak. 1:27). 7. Usitoe ili kuonekana na watu: mkono wako wa kushoto usijue ufanyolo mkono wa kuume (Mt. 6:1-4). 8. Usimlipe mtu maovu kwa maovu: shinda maovu kwa kutenda mema (Rum. 12:17-21). 9. Wabariki wanaokulaani: laana isitoke kinywani mwako (Mt. 5:44; Rum. 12:14). 10. Usilipe maovu kwa maovu, au matusi kwa matusi, bali ubariki tu (1 Pet. 3:9). 11. Waombee hao wanaokudharau na kukutesa (Mt. 5:44). 12. Usiwe na chuki; usihukumu; usinung'unike; usiwakatie wengine kesi (Yak. 5:9; Mt. 7:1). 13. Tupilia mbali hasira, gadhabu, uchungu, na kila usemi wa uovu (Efe. 4:31; 1 Pet. 2:1). 14. Chukulianeni shida senu (Yak. 5:16). 15. Usishiriki ya dunia: usipende mambo ya ulimwengu (Rum. 12:2; 1 Yoh. 2:15). 16. Katalia mbali mambo yasiyo ya Mungu na tama za ulimwengu. Mkono unaokusumbua, ukate (Tito 2:12; Mt. 5:30). 17. Watumishi, iweni waaminifu hata kwa mabwana wabaya (Efe. 6:5-8). 18. Usiyafikirie mambo ya juu, bali toshekeni na mambo ya watu yakhe (Rum. 12:16). 19. Usiwe na deni la mutu awaye yote (Rum. 13:7-8). 20. Kutitokea dhambi (inayojulikana au kusikika), usiwambie wengine, bali mwambie ndugu aliyekosa juu ya jambo hilo kati yako naye peke yenu, kusudi ni kurekebisha (Mt. 18:15; Gal. 6:1). 21. Mpwende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote (Mt. 22:37). 22. Omba kila mara; omba kwa ufupi bila mambo mengi: omba kwa siri (Luka 18:1; Mt. 6:7). 23. Katika kila jambo, mshukuru Mungu na umtambue katika njia zako zote (Efe. 5:20; Mit. 3:6). 24. Jinsi mnavyotaka watu wawatendeeni ninyi, nanyi watendee vile vile (Mt. 7:12). 25. Chukua mfano wa Kristo na ufuate nyayo zake (1 Pet. 2:21). 26. Kristo na Adamu mioyoni mwenu kwa imani (Efe. 3:17). 27. Kristo na awe zaidi ya vitu vyote unavyovitaka duniani: naam, zaidi ya uhai wako (Luka 14:26). 28. Mkiri Kristo waziwazi mbele ya watu (Luka 12:8). 29. Jihadhari, mahitaji ya maisha na mvuto wa anasa usilegeze upendo wake kwako wewe (Luka 21: 34-36; Mt. 24:44). 30. Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe (Mt. 22:39). 31. Usiew bwana mkubwa juu ya ye yote (Mt. 23:10-12). 32. Usijifikirie kibinafsi, wala kujitatulia matatizo yako tu, bali waangalie na wengine (Fil. 2:4; Gal. 6:2). 33. Nuru yako na iangaze mbele ya watu: lishike vema neno la uzima. Watendee watu wote mema ukiwa na nafasi (Mt. 5:16; Fil. 2:16; Gal. 6:10). 34. Ishi bila lawama na usimdhuru mtu, kama wana wa Mungu katikati ya kizazi kiovu na kilichopotoka (Fil. 2:15). 35. Uwe mngwana, mpole, mwenye moyo safi, rehema, huruma, mwenye kusamehe (2 Tim. 2:24; Tito 2:2; Efe. 4:32). 36. Uwe na kiasi, usichukulie mambo hivi hivi, uaminike, uwe kadiri (Fil. 4:5; 1 Pet. 1:13; 5:8). 37. Semeni ukweli kila mtu na jirani wake: epukana na uongo wa kila namna (Efe. 4:25). 38. Cho chote mfanyacho, kifanye kama kwamba wamfanyia Bwana, wala sio wanadamu (Kol. 3:23). 39. Kesha, uwe macho jasiri, mwenye furaha, adabu njema na tenda kiume (1 Kor. 16:13; Fil. 4:4; 1 Thes. 5:6-10). 40. Jivike upole: uwe na saburi kwa watu wote (Kol. 3:12; Rum. 12:12). 41. Ishi kwa amani na watu wote (Ebr. 12:14). 42. Shiriki furaha na huzuni ya wengine (Rum. 12:15). 43. Yafuate yote yaliyo ya kweli, haki, safi, kupendeza, sifa nzuri, wema, na kusifika (Fil. 4:8). 44. Jiepushe kabisa na uzinzi, uasherati, uchafu, ulevi, tama, ghadhabu, mashindano, uasi, chuki, uigaji, kujidai, kujipendekeza, wivu, mzaha na maongezi ya upuzi (Efe. 5: 3-4). 45. Lo lote utendalo, fikiria matokeo yake katika kulitukuza Jina la Mungu kati ya watu. Yote yafanyike kwa utukufu wa Mungu (1 Kor. 10:31; Kol. 3:17). 46. Jihesabuni wafu kwa dhambi ya kila namna. Tangu sasa ishini kwa sababu ya yule aliyekufa kwa ajili yenu na kufufuka tena (Rum. 6:11;2 Kor. 5:15). 47. Usichoke katika kutenda mema, ukitenda kazi ya Bwana (Tito 2:14; Gal. 6:9). 48. Usiseme maovu juu ya mtu awaye yote (Tito 3:2). 49. Neno la Kristo na likae ndani yenu (Kol. 3:16). 50. Uneni wenu uwe wa kupendeza, utiliwe chumvi kiasi (Kol. 3:8; 4:6). 51. Tii watawala; tii kila mamlaka kwa ajili ya Bwana (Tito 3:1). 52. Mazungumzo yako yote yawe ya kupendeza (1 Pet. 1:15-16). 53. Usimpe adui nafasi kusema mabaya juu yako (1 Tim. 5:14). |