toleo la kirafiki la simu bonyeza hapa

                                                Tamko ya Imani

                                                    kutengeneza

                                           msingi wetu wa ushirika

 

                                           A Statement of The Faith

                                     forming our Basis of Fellowship

 

                                                                   pamoja        

                                     na Mafundisho ya Kukataliwa

                                                na Amri za Kristo

 

                                  including Doctrines to be Rejected

                                    & the Commandments of Christ

 

 

MSINGI -

 

Kuwa   kitabu   kijulikanacho   kama Biblia, chenye  Maandiko ya Musa, Manabii, na Mitume, ndicho chenye elimu  au habari kuhusu Mungu na nia Yake wakati huu au ipatikanayo duniani, na kimetokana uongozi wa pumzi ya Mungo takita waandishi, na haina    kosa    lotote katika   sehemu    zote, isipokuwa makosa ambayo yaweza kupatikana kutokana na kunakili vibaya au tafsiri (2 Tim. 3:16; 1 Kor. 2:13; Ebr. 1:1; 2 Pet. 1:21; 1 Kor. 14:37; Neh. 9:30; Yoh. 10:35).

 

UKWELI  KUPOKELEWA -

 

I-Kuwa Mungu wa pekee wa  kweli ni yule aliyefunuwila kwa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, kwa kutokea malaika,  na kwa Musa  kupitia kwa mwali wa moto ambao haukuteketeza  kijiti  na  pia  kwenye mlima  wa Sinai, na aliyejifinua Mwenyewe  katika Bwana Yesu Kristo, kama  Mungu  mkuu aishie kwa uwezo wake mwenyewe,  BABA MMOJA, aishiye katika nuru isiwoyeza kukaribiwa, lakini yuko kilamahali kwa Roho Yake, ambayo ni sehemu ya nafsi Yake, mbinguni. Kwa uwezo wake mwenyewe, ameumba mbingu na nchi, na vyote vilivyomo (Isa. 40:13-25; 43:10-12; 44:6-8; 45:5; 46:9-10;   Ayubu 38, 39 na 40; Kumbu. 6:1-4;  Marko 12:29-32;  1 Kor. 8:4-6;  Efe. 4:6; 1 Tim. 2:5;   Neh. 9:6; Ayubu 26:13; Zab. 124:8;  146:6; 148:5;  Isa. 40:25-27; Yer. 10:12-13; 27:5; 32:17-25; 51:15; Mdo. 14:15; 17:24;  1 Nya. 29:11-14; Zab. 62:11; 145:3; Isa. 26:4; 40:26; Ayubu 9:4; 36:5; Zab. 92:5; 104:24; 147:4-5; Isa. 28:29;  Rum. 16:27;  1 Tim. 1:17; 2 Nya. 16:9; Ayubu 28:24; 34:21; Zab. 33: 13-14; 44:21; 94:9; 139:7-12; Mit. 15:3; Yer. 23:24; 32:19; Amosi 9:2-3; Mdo 17:27-28; Zab. 123:1; 1 Fal. 8:30-39, 43, 49; Mt. 6:9; 1 Tim. 6:15-16; 1:17).

 

II-Kuwa  Yesu  wa  Nazareti  alikuwa Mwana  wa  Mungu, aliyezaliwa  na Bikira Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, bila mwingilio wa mtu mume, na baadaye akapewa roho yule pasipo kipimo, wakati wa ubatizo wake (Mt. 1: 23; 1 Tim. 3:16; Mdo. 2: 22-24, 36; Mt. 1:18-25; Luka 1:26-35; Gal. 4:4; Isa. 7:14; Mt. 3:16-17; Isa. 11:2; 42:1; 61:1;  Yoh. 3:34; 7:16; 8:26-28; 14:10-24).

 

III-Kuwa kufunuliwa kwa Yesu wa Nazareti duniani kulihitajika kwa sababu ya mahali na hali walimokuwemo binadamu kwa ajili va mambo yaliyohusia na mtu wa kwanza (1 Kor. 15:21-22; Rum. 5:12-19; Mwa. 3:19; 2 Kor. 5:19-21).

 

IV-Kuwa mtu wa kwanza alikuwa Adamu, aliyeumbwa na Mungu kutoka kwa mavumbi ya ardhi kama nafsi hai, au mwili wa kawaida wenye uhai, hiki kilichoumbwa kilikuwa "chemasana" kwa namna na hali, na akawekwa chini ya sheria ambayo kwayo kuendelea kwa uhai kurgetegemea utii (Mwa 2:7; 18:27; Ayubu 4:19; 33:6; 1 Kor. 15:46-49; Mwa. 2:17).

 

V-Kuwa Adamu aliijunja sheria hii, na akahukumiwa kuwa hafai kuwa na uzima wa milele, na akahukumiwa kurudi ardhani alikotolewa -hukumu ilyomnajisi au kumchafua na ikawa sheriaya hali yake ya kimwili, na ikapitishwa kwa uzao wake wote (Mwa. 3:15-19, 22-23; 2 Kor. 1:9; Rum. 7:24; 2 Kor. 5:2-4; Rum. 7:18-23; Gal. 5:16-17; Rum. 6:12; 7:21; Yoh. 3:6; Rum. 5:12; 1 Kor. 15:22; Zab. 51:5; Ayubu 14:4).

 

VI-Kuwa Mungu kwa huruma Yake, alibu  ni mpango wa kurudisha hali ya kwanza ambayo, bila kuweka kando sheria yake ya haki na ipasayo dhambi na mauti, mwishowe ingemwokoa mwanadamu kutoka kwa maangamizi, na dunia ijazwe na watu wenye kuishi milele bila dhambi (Ufu.21:4; Yoh. 3:16; 2 Tim. 1;10; 1 Yoh. 2:25; 2 Tim. 1:1; Tito 1:2; Rum. 3:26; Yoh.1:29).

 

VII-Kuwa Alianzisha mpango huu mpango huu kwa kutoa ahadi kwa Adamu, Ibrahimu na Daudi, na baadaye akaueleza vizuri zaidi kupitia kwa manabii (Mwa. 3:15; 22:18; Zab. 89:34-37; 33:5; Hos. 13:14; Isa. 25:7-9; 51:1-8; Yer. 23:5).

 

VIII-Kuwa miadi hii ilikuwa na maana au kiini kwa Yesu Kristo, ambaye angetokana na uzao uliohukumiwa wa Ibrahimu na Daudi, na ambaye, ingawa alikuwa amevikwa hali yao ya hukumu, angepata nafasi ya ufufuo kwa kutii kabisa, na, kwa kufa afutilie mbali sheria ya hukumu hiyo kwa nafsi yake na kwa wote amboa wangemwamini na kumtii (1 Kor. 15:45; Ebr. 2:14-18; Rum. 1:3; Ebr. 5:8-9; 1:9; Rum. 5:19-21; Gal. 4:4-5; Rum. 8:3-4; Ebr. 2:15; 9:26; Gal. 1:4; Ebr. 7:27; 5:3-7; 2:17; Rum. 6:10; 6:9;  Mdo. 13:34-37; Ufu. 1:18; Yoh. 5:21-22, 26-27; 14:3; Ufu. 2:7; 3:21; Mt. 25:21; Ebr. 5:9; Marko 16:16; Mdo. 13:38-39; Rum. 3:22; Zab. 2:6-9; Dan. 7:13-14; Ufu. 11:15; Yer. 23:5; Zek. 14:9; Efe. 1:9-10).

 

IX-Kuwa ni kazi hii iliyosababisha kuzaliwa kwake Kristo kimuujiza na mama wa kibinadamu, akaweza kujitwika mzigo wa hukumu yetu, na, kwa wakati huo huo, akawa mwenyewe hana dhambi, na kwa hivyo, akawa na uwezo wa kuinuka kutoka kwa mateso ya mauti iliyohitajika wema au haki yake Mungu (Mt. 1:18-25; Luka 1:26-35;  Gal. 4:4; Isa. 7:14; Rum. 1:3-4; 8:3; 2 Kor. 5:21; Ebr. 2:14-17; 4:15).

 

X-Kuwa akiwa mzaliwa wa Mungo hivyo, akiwa ndani yake na kutumiwa na Mungu kupitia kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani, Yesu alikuwa Imanueli, Mungu pamoja nasi, Mungu aliyefunuliwa katika mwili - ingawa katika maisha yake ya kibinadamu, alikuwa na maumbile sawa na mtu asiye na maisha na milele, mtu wa kufa, aliyetokana na mwanamke, wa nyumba na mbari ya Daudi, na kwa hivyo mwenye mateso, katika siku zake za mwili, kutokana na matokeo ya makosa ya Adamu, ikiwemo mauti iliyowajia watu wote, aliyoshiriki kwa kuwa maubile yaliyofanana nao (Mt. 1:23; 1 Tim. 3:16; Ebr. 2:14; Gal. 4:4; Ebr. 2:17).

 

XI-Kuwa ujumbe aliouleta kwa watu wa kwake, yaani Wayahudi, kutoka kwa Mungu, ulikuwa ni wakuwaita waje watubu na waache kazi zote za uovo, madai yake juu ya wana uliotakana na uungu na utawala wake juu ya Wayahudi; na kutangazwa kwa habari njema kuwa Mungu atawarudishia ufalme kupitia kwake, na kuyatimiza yote yaliyoandikwa katika manabii (Marko 1:15; Mt. 4:17; 5:20-48; Yoh. 10:36; 9:35; 11:27; 19:21; 1:49; Mt. 27:11-42; Yoh. 10:24-25; Mt. 19:28; 21:42-43; 23:38-39; 25:14 mpaka mwisho; Luka 4:43; 13:27-30; 19:11-27; 22:28-30; Mt. 5:17; Luka 24:44).

 

XII-Kuwa kwa kutoa ujumbe huu, aliuawa na Wayahudi na Warumi, ambao walikuwa, kwa vyo vyote vile, vyombo vilivyotumiwa na Mungu, kutimiza kazi iliyoazimiwa tangu hapo - kuharibiwa  kwa  dhambi  katika mwili, kupitia kwa mwili wa Yesu kutolewa mara moja tu, kama kipatanisho kutangaza wema wa Mungu, kama msingi wa ondoleo la dhambi. Wote wanaomwendea Mungu kupitia kwake huyu aliyesulubiwa, lakini aliyefufuka, mjumbe wa uzao wa Adamu ulioasi, husamehewa. Kwa hivyo, kwa mfano, damu yake yatutakasa kutoka kwa dhambi (Luka 19:47; 20:1-16; Yoh. 11:45-53; Mdo. 10:38-39; 13:26-29; 4:27-28; Rum. 8:3; Ebr. 10:10; Rum. 3:25; Mdo. 13:38; 1 Yoh. 1:7; Yoh. 14:6; Mdo. 4:12; 1 Pet. 3:18; 2:24; Ebr. 9:14; 7:27; 9:26-28; Gal. 1:4; Rum. 3:25; 15:8; Gal. 3:21-22; 2:21; 4:4-5; Ebr. 9:15; Luka 22:20; 24:26, 46-47; Mt. 26:28).

 

XIII-Kuwa siku ya tatu, Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, na akampandisha mbinguni ili awe kuhani mpatanishi kati ya Mungu na binadamu, katika jitihada ya kuwakusanya kati yao watu ambao wafaa kuokolewa kuamini na kutii ukweli (1 Kor. 15:4; Mdo. 10:40; 13:30-37; 2:24-27).

 

XIV-Kuwa yeye ni kuhani juu ya nyumba yake mwenyewe tu, na haombei ulimwengu mzima, au wale wanaojidai kuwa wake hali wametupwa kwa ajili ya kutotii. Kuwa huwasaidia ndugu zake wanaokosea,  wanapokiri na kuziacha dhambi zao (Luka 24:51; Efe. 1:20; Mdo. 5:31; 1 Tim. 2:5; Ebr. 8:1; Mdo. 15:14; 13:39; Ebr. 4:14-15; Yoh. 17:9; Ebr. 10:26; 1 Yoh. 2:1; Mit. 28:13). 

 

XV-Kuwa aliwatuma mitume wakatangaze wokovu katika yeye, jina la pekee chini ya mbingu kwalo wanadamu wapate kuokolewa (Mdo. 1:8; Mt. 28:19-20; Luka 24: 46-48; Mdo. 26:16-18; 4:12).

 

XVI-Kuwa njia ya kupokea wokovu huu ni kwa kuamini injili waliyoihubiri, na kulichukua jina na kufanya kazi ya Kristo, kwa kuzikwa majini, na kuendelea kwa saburi katika kuyashika maagizo yote aliyoamuru, na ye yote asihesabike kuwa rafiki yake isipokuwa wale tu wanaoyatimiza aliyoamuru (Mod. 13:48; 16:31; Marko 16:16; Rum. 1:16; Mdo. 2:38, 41; 10:47; 8:12; Gal. 3:27-29; Rum. 6:3-5; 2:7; Mt. 28:20; Yoh. 15:14).

 

XVII-Kuwa injili ni mambo yanayohusu "ufalme wa Mangu na Jina lake Yesu Kristo" (Mdo. 8:12; 19:8, 10, 20; 28:30, 31).

 

XVIII-Kuwa mambo ya Ufalme wa Mungu ni mambo bayana yaliyoshuhudiwa kuhusu Ufalme wa Mungu katika maandishi ya manabii na mitume, kama inavyoelezwa katika mufungu an aya kumi na mbili zifuatozo.

 

XIX-Kuwa Mungu atausimamisha ufalme duniani, ufalme ambao utaangusha falme zingine zote, atazigeuza kuwa "ufalme wa Bwana wetu na Kristo wake" (Dan. 2:44; 7:13, 14; Ufu. 11:15; Isa. 32:1, 6; 2:3, 4; 11:9, 10).

 

XX-Kuwa kwa sababu hii Mungu atamtuma Yesu Kristo mwenyewe hapa duniani mwisho wa siku za watu wa Mataifa (Mdo. 3:20, 21; Zab. 102:16, 21; 2 Tim. 4:1; Mdo. 1:9, 11; Dan. 7:13).

 

XXI-Kuwa ufalme atakaousimamisha utakuwa ufalme wa Israeli utakaorudishwa, katika nchi ile ile ufalme huo ulipokuwa hapo awali, yaani, nchi iliyopewa Ibrahimu kama urithi wa milele na kwa uzao wake (Kristo) kwa agano (Mika 4:6-8; Amosi 9:11, 15; Ezek. 37:21, 22; Yer. 23:3, 8; Mwa. 13:14, 17; Ebr. 11:8, 9; Gal. 3:16; Law. 26:42; Mika 7:20).

 

XXII-Kuwa kurudishwa kwa ufalme kwa Waisraeli kutasababisha kukusanywa kwa wateule wake Mungu lakini taifa lililotawanyika, Wayahudi; watapandwa tena katika nchi ya baba zao, itakapokuwa imekombolewa kutoka kwa "Ukiwa wa vizazi vingi"; kujengwa tena kwa Yerusalemu uwe "kiti cha enzi cha Bwana" na mji mkuu ulimwenguni kote (Isa. 11:12; Yer. 31:10; Zek. 8:8; Ezek. 36:34, 36; Isaya 51:3; 60:15; 62:4; Yer. 3:17; Mika 4:7, 8; Yoeli 3:17; Isa. 24:23).

 

XXIII-Kuwa watawala wa ufalme huo utakaokuwa umeimarishwa watakuwa nudugu zake Kristo, wa vizazi vyote, ambao watatokana na ufufuo na kugeuzwa kwao, na kusanyiko, wakiwa pamoja na Kristo kama kiongozi wao, mkusanyiko wa "uzao wa Ibrahimu", ambaye katika yeye mataifa yote yatabarikiwa, wakiwemo "Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, na manabii wote", na wote katika vizazi vyao waliokuwa na uaminifu kama wao (Dan. 12:2; Luka 13:28; Ufu. 11:18; 1 The. 4:15-17; Yoh. 5:28, 29; 6:39, 40; Luka 14:14; Mt. 24: 34, 46).

 

XXIV-Kuwa atakapofunuliwa au kuja Kristo, na kabla ya ufalme kusimamishwa, wale wenye kuaminishwa au kutadiriki (yaani, wale wanaofahamu mapenzi yake Mungu, na wameitwa kujishughulisha na kazi hiyo), waliokufa na walio hai - watiifu na wasio tii - wataitwa mbele ya kiti chake cha hukumu "kuhukumiwa kulingana na kazi zao" na "kupokea ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya" (2 Kor. 5:10; 2 Tim. 4:1; Rum. 2:5, 6, 16; 14:10-12; 1 Kor. 4:5; Ufu. 11:18).

 

XXV-Kuwa wasio waaminifu watakuwa katika aibu na "mauti ya pili",na maaminifu watavikwa kutoharibika, miili ya kuishi milele, na kupewa heshima ya kutawala pamoja ya Yesu kama warithi pamoja naye wa ufalme, warithi nchi pamoja, na washiriki usimamizi wa mamlaka yake Mungu kati ya watu katika kila jambo (Mt. 7:26; 8:12; 25:20; Dan. 12:2;  Gal. 6:8; 5:21; 2 Thes. 1:8; Ebr. 10:26-28; 2 Pet. 2:12; Ufu. 21:8; Mal. 4:1; Zab. 37:30-38; Mit. 10:25-29; 1 Kor. 15:51-55; 2 Kor. 5:1-4; Yak. 1:12; Rum. 2:7; Yoh. 10:28; Mt. 5:5; Zab. 37:9, 22, 29; Ufu. 5:9; Dan. 7:27; 1 Thes. 2:12; 2 Pet. 1:11; Ufu. 3:21; 2 Tim. 2:12; Ufu. 5:10; Zab. 49:7-9; Luka 22:29-30).

 

XXVI-Kuwa Ufalme wa Mungu, ukiwa hivi, utaendelea kwa miaka elfu moja, katika muda huo dhambi na mauti itaendelea kati ya raia wa nchi, ingawa ni kwa kiwango cha chini sana kuliko wakati huu (Ufu. 20:4; 11:15; Isa. 65:20; Ezek. 44:22, 25; 1 Kor. 15:24,28).

 

XXVII-Kuwa sheria itaimarishwa itakayowaendea mataifa yote ili "ikwafunze haki", matokeo yake yatakuwa kumalizwa kwa vita duniani; na "dunia itajazwa maarifa ya utukufu wa Bwana, kama maji yaifunikavyo bahari" (Mika 4:2; Isa. 42:4; 11:1-5; 2:2-4; Hab. 2:14).

 

XXVIII-Kuwa juhudi ya Ufalme itakuwa kuwaangamiza adui wote, na hatimaye mauti yenyewe, kwa kuwafungulia mataifa yote njia ya uzima, ambayo wataingia kwa imani, katika miaka hiyo elfu moja, na (haswa) mwisho wake (1 Kor. 15:25-26; Ufu. 21:4; 20:12-15; Isa. 25:6-8).

 

XXIX-Kuwa mwisho wa miaka elfu moja, kutakuwepo na ufufuo na hukumu ya jumla, matokeo yake ni kuangamizwa kwa waovu wote, na kupewa uzima wa milele wale ambao watakuwa wamejipatia jina la sifa (chini ya neema ya Mungu) ya kuishi milele katika hiyo miaka elfu moja (Ufu. 20:11-15; 1 Kor. 15:24).

 

XXX-Kuwa serikali itatolewa na Yesu, apewe Baba, atakayejifunua kama "yote kwa wote"; dhambi na kifo vimeondolewa, na mbio zimerejeshwa kabisa kwa urafiki wa Mungu (1 Kor. 15:28).

 

                                                           mbili   faharasa